Biashara nyingi zimekuwa zikifa pindi Tu zinapoanzishwa, kipindi cha MWANZO katika biashara mara nyingi kinakuwa kigumu Sana kwa waanzilishi WA biashara
Leo nakupa kanuni 5 muhimu unazo takiwa zifuata ili hiyo biashra yako au kitu unacho taka kuanzisha kiwe na mwendelezo mzuri kabisa.
01. Kuelewa Soko,
Kabla Hujaingia Katika Kufanya Biashara Kubwa Hakikisha Kwamba Unalielewa Soko Vizuri Sana. Hakikisha Unafahamu Wateja Wako Ni Watu Wa Aina Gani, Wanatoka Wapi, Fahamu Umri Pamoja Na Changamoto Zao.
02. Ubunifu Na Kujielekeza,
Kama Unataka Biashara Yako Isife Katika Kipindi Cha Miaka Miwili Kua Tayari Kua Mbunifu Na Kua Tayari Kujiendeleza. Biashara Nyingi Sinakufa Zaidi Kwa Hiki Kipindi Cha Karibuni Waanzilishi Wake Hawataki Mabadiliko Kabisa.
03. Mipango Mizuri,
Andaa Mipango Mizuri Inayotekelezeka Katika Ukuaji Wa Biashara Yako Kwani Mipango Mizuri Ndio Chanzo Cha Mafanikio Katika Biashara Yako. Biashara Itakutoa Ndani Ya Miaka Miwili Iwapo Utaianzisha Bila Mipango Mizuri Yakuiongoza!
04. Nidhamu Ya Fedha,
Hapa Ndipo Wengi Wanapoanguka Katika Biashara Zao. Nidhamu Ya Fedha Ni Kitu Cha Muhimu Sana Katika Biashara. Hakikisha Unapata Mgawanyo Sahihi Kwa Ajili Ya Mtaji, Akiba Na Faida Unayopata Ili Kuongeza Ukubwa Wa Biashara Yako.
05. Ajiri Watu Sahihi,
Biashara Inapaswa Kuongozwa Na Watu Sahihi Hivyo Jitahidi Katika Kutoa Ajira Kwa Watu Sahihi. Kama Ukiajiri Watu Sahihi Katika Biashara Yako Au Huduma Yako Itakupa Nafasi Ya Wewe Kufanikiwa Zaidi, Ila Usipopata Watu Sahihi Hilo Ni Anguko Lako.
