WETCU WAWEKEZA HISA ZA KIBIASHARA CRDB NA KUNUNUA HATI FUNGANI KUONGEZA MTAJI NA MAPATO.



SMC-TABORA.

Ili kuongeza Mapato na Mtaji wa Chama Kikuu cha Ushirika WETCU 2018 LTD,kimewekeza Hisa za kibiashara CRDB bank, Ushirika Tower na Cooperative Bank of Tanzania zenye thamani ya Sh19,360,000,000.


Mwenyekiti wa Bodi ya WETCU 2018 LTD Hamza Kitunga ameiambia Serengeti Media Centre na Antoma Tv Online kuwa,katika Ushirika Tower wamenunua hisa zenye thamani ya Sh50 milioni,CRDB Bank zenye thamani 18,720,000,000,Cooperative Bank of Tanzania wamenunua hisa za Sh590,000,000.


”Hii inatusaidia kupata mapato ya ziada kupitia mgao wa faida,pili mtaji wa chama unaongezeka hasa bei ya hisa inapopanda,inaongeza thamani ya uwekezaji ya chama,pia ni uwekezaji salama wa muda mrefu ,maana tukimiliki hisa nyingi tunaweza kuwa na sauti kwenye mikutano ya wana hisa,”amesema.


Amesema,wanahisa 24,000,000 katika benki ya CRDB ambazo kufikia Machi 31,2025 zilikuwa na thamani ya Shs 18,720,000,000,wakati huo bei ya hisa za CRDB kwenye soko kufikia tarehe 28 Machi 2025 ilikuwa ni sh 780 kwa hisa. 


Kitunga amesema,pia Chama Kikuu kina Hisa 10,000 zenye thamani ya Sh 50,000,000 kwenye Jengo la Ushirika Tower lililopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam,hata hivyo  chama na wanahisa wengine, hawajaanza kupata gawio la faida kwa kuwa mradi huo haujaanza kutoa faida tangu uanze. 


Amesema,wanampango wa kununua hisa zaidi CBT na Treasury Bond ya BoT,ikiwemo kununua hisa Cooperative Bank Of Tanzania (CBT)”pamoja na mipango hiyo,Chama Kikuu kiliwekeza Hisa 1,180,000 zenye thamani ya sh590,000,000,”amesema na kuongeza, 


“Kwenye Benki ya Ushirika Tanzania (CBT)tunategemea kuongeza ununuzi wa hisa 150,000 zenye thamani ya sh75,000,000 ili tuweze kufikisha hisa 1,330,000 toka hisa 1,180,000 zilizopo sasa,amesema.


Meneja Mkuu wa WETCU 2018 Samwel Jokeya amesema,wanategemea kununua hati fungani ya BoT za muda wa miaka 25 zenye thamani ya Sh310,000,000 ambazo zitawapatia faida kiasi cha Sh 48,825,000 kwa mwaka  kwa kiwango cha asilimia 15.75.


Amesema,wana hisa kwenye Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC)za uanachama zenye thamani ya Sh30Milioni,na Kampuni ya FDTU na TCJE Ltd,”pia tumewekeza kiasi cha sh100milioni katika akaunti ya muda maalum (Fixed Deposit) katika benki ya EXIM,Chama kina pata faida ya asilimia 8 kwa mwaka,”amesema.


Faida kwa wanachama amesema,inawasaidia kujenga tabia  ya kuwekeza katika rasilimali zinazotoa faida,pia uwezo wa kuuza ikiwemo kujifunza kuhusu masoko ya mitaji,usimamizi wa fedha na mikakati ya kifedha,na inahamasisha shughuli za chama.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi